Saturday, December 21, 2013

TCRA YAWAFUNDA WAANDAAJI WA VIPINDI NA WATANGAZAJI WA REDIO KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi, Injinia Magreth Munyagi amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha watangazaji kuhusu kufuata maudhui yaliyokusudiwa yanayoelimisha na kuburudisha jamii na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Kushoto ni Mgeni rasmi wa Warsha hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha, na kulia ni mjumbe wa Bodi ya TCRA, Bw. Joseph Mapunda

Mgeni rasmi wa Warsha hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amesema kukiuka kwa maadili katika baadhi ya vituo vya utangazaji kunatokana na wamiliki kuwaajiri wafanyakazi wasiokuwa na taaluma ya Utangazaji. Kushoto ni mjumbe wa Bodi ya TCRA Bw. Walter Bgoya.

Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mbeya MhandisDeogratius Moyo wana warsha kuchangia mada

Frederick  Ntobi Naibu Mkurugenzi idara ya utangazaji Mamlaka ya mawasiliano akiwafunda waandaaji wa vipindi  na watangazaji wa radio kanda ya nyanda za juu kusini


Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy akiongoza mijadala katika Warsha ya Siku Mbili kwa kwa waandaaji wa vipindi na watangazaji wa Radio



Baadhi ya watangazaji wakichangia mada


Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment