Saturday, January 18, 2014

Waziri Profesa Sospeter azindu warsha ya uzinduzi wa mfumo wa Utafiti wa Geofizikia Data jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wadau wa sekta ya madini (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya uzinduzi wa Mfumo wa Utafiti wa Geofizikia data jana  jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Kampuni ya Geotech Airborne Limited Malcolm Moreton akielezea namna kampuni yake ilivyoshirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha mfumo wa Utafiti wa Geofizikia unafanikiwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Geological Survey Tanzania (GST), Abdulkarim Mruma akifafanua jambo wakati wa warsha ya uzinduzi Mfumo wa Utafiti wa Geofizikia data jana  jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya Jeolojia wakifuatilia mada kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Geological Survey Tanzania (GST), Abdulkarim Mruma (hayupo pichani), jana  jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha ya uzinduzi wa mfumo wa Utafiti wa Geofizikia Data iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benjamin Sawe - MAELEZO)

No comments:

Post a Comment