
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa
na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu
vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi
unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari
Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia)
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula akizungumza na mhudumu
wa afya katika wadi ya wazazi Samazi juu ya huduma na mahitaji ya kituo
hicho kipya ambacho kinategemewa kuanza kazi siku za hivi karibuni.


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimkaribisha Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula katika Wilaya yake kwa
ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki la
Kirando linalofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika uliopo
chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.



Gati linaloendelea kujengwa kwa ajili yakuhudumia soko hilo la samaki la Kirando wilayani Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment