Ndege
mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale
waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko
mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.
Theluthi
mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na
nchi hiyo iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko
nusu mlingoti.
Mfalme
na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven
pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.
Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.
Vifaa
vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa
Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .
Maafisa
wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi
waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu
tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi
wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka
na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
No comments:
Post a Comment