Timu zote mbili kati ya Kitendaguro Fc na Rwamishenye Fc wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza
Kikosi cha Timu ya Rwamishenye Fc kilichoanzakikosi cha Timu ya Kitendaguro Fc (Makhirikhiri).
TIMU
ya Kitendaguro Fc Maarufu kwa jina la Makhirikhiri wamewanyoosha wenzao
nao wanaojulikana zaidi kama Wanabodaboda Rwamishenye Fc kwa Mikwaju ya
penati 6-5 baada ya kutoshana nguvu katika dakika 90 ya bila kufungana! Mashabiki
wa Timu mbili hizi kati ya Rwamishenye Fc na Kitendaguro walishindwa
kuamini kile kilichotokea machoni mwao, Wakijionea kila timu ikishindwa
kuliona lango la mwenzake huku kabla ya Mtanange kila mmoja alikuwa
akijigamba kukwepa kwenda hatua ya Mikwaju ya penati!
Mapema
Kipindi cha kwanza hakuna aliyeliona lango la mwenzake katika dakika 45
za kipindi hicho nacho kipindi cha pili pamoja na Mtanange kushika kasi
za mashabulizi ya hapa na pale timu zote zilibanana na kuweza kumaliza
dakika 90 ya bila kufungana na Hatimae Mikwaju ya Penati kuamua nani wa
kukamilisha timu nne za Nusu Fainali. Mikwaju ya Penati ilipigwa saba na
hatimae Timu ya Rwamishenye kukosa 2 na Kitendaguro kukosa 1 hivyo
Makhirikhiri kusonga hatua ya Nusu Fainali.
Mashindano
haya ya Ligi ya Kagasheki yataendelea hapo kesho kwa Nusu Fainali ya
Kwanza kati ya Mabingwa watetezi Bilele Fc na Miembeni Fc.Kukaba ilikuwa ni mpango mzima Mchezaji
wa Rwamishenye Fc Maximilian Thadeo (kushoto) akikabwa vilivyo na
wachezaji wawili wa Kitendaguro Khamis na Timu kapteni Mchezo ulikuwa wa kasi sana katika kipindi cha kwanza kila mmoja akitaka kumwondoa mwenzake mapema.Mapema
Mashabiki walikuwa wameishajichukulia nafasi zao katika Uwanja wa
Kaitaba si Jukwaa kuu wala majukwaa madogo..saa tisa kamili nyomi
ilishashona!!!Mambo ya Mizuka ya ligi hii ya Kagasheki 2014, Leo hata Vuvuzela zilipigwa!Nyomi ya Mashabiki Jukwaa Dogo!Mashabiki Wakina Mama nao hawakuwa nyuma!! Leo ndani ya Kaitaba!Viongozi
wa Timu ya Kagera Suagar ya Hapa Bukoba nao walikuwepo kaitaba
Uwanjani!! katikati noi Kocha Msaidizi wa Timu ya Kagera Sugar
inayoshiriki Ligi kuu Vodocom na kulia ni Bw. Mwamed.Khamis
(kulia) wa Timu ya Kitendaguro akipanga amtoke vipi Straika wa
Rwamishenya Edwin Issack(kushoto) katika kipindi cha kwana.Seleman Khamis wa Rwamishenye akifanya mashambulizi Mwisho wa yote alikutana na ngome kali ya beki wa Kitendaguro safari ikaishia hapo!Seleman Hamis alisumbua sana ngome ya KitendaguroHapa sasa hutoki!!Mbele ya Mwamuzi vijana wakichuana huku Mwamuzi akiwasoma!Rwamishenye waliotea bao hapa na Mwamuzi wa pembeni akawapiga kibendera!Mashabiki wa Rwamishenye wamekosa nafasi wakaamua Bodaboda zao kuwa sehemu ya kiti!Dakika 90 tuazimaliza hivi hivi !! ndio maana tunaitwa Wanabodaboda wa Rwamishenye!!Mashabiki leo waliingia kwa Wingi kushuhudia Kipute nani anahitimisha nafasi ya Nne kwenda Nusu fainali.Mikwaju
ndio iliwatoa Rwamishenye na hapa ni kipa wake akipelekeshwa katika
mkwaju wa Mwisho!! mpira umepigwa huku yeye akajitupa kule!!Wachezaji
wa Kitendanguro wakishangilia kwenda Nusu Fainali baada ya kuwatoa
kamasi Wanabodaboda timu ya Rwamishenye Fc penati 6-5kushoto ni kipa wa Makhirikhiri Kitendaguro Fc akifurahia ushindi na mwenzakeUshindi Mtamu!!! tunaenda Nusu Fainali!!!Dada Shabiki wa Timu ya Kitendaguro alishindwa kujizuia akajikuta katikati ya Uwanja!!
No comments:
Post a Comment