Wednesday, July 23, 2014

Kocha wa Kenya aadhibiwa na CAF




Kocha Adel atakosa mechi kwa mwaka mmoja
Katibu wa shirikisho la kandanda la Kenya, FKF, Mike Esakwa amemtetea kocha wa timu ya raifa ya Kenya dhidi ya tuhuma za kukosa maadili.
Shirikisho linalosimamia soka Afrika, CAF,limempiga marufuku kocha Adel Amrouche kwa mwaka mmoja kwa madai kuwa alimtemea mate mmoja ya maafisa waliosimamia mechi kati ya Harambee Stars ya Kenya na wenyeji Comoros mwezi jana.
Katibu wa CAF Hicham El Amrani amesema kulingana na sheria zao adhabu ya kosa kama hilo ni kufungiwa miezi kumi na mbili.
Lakini katibu wa FKF Esakwa amesema:''Tunajiandaa kukata rufaa kwa siku tatu zijazo kwa sababu huo ni uongo mtupu! Mimi nilikua Comoroa sikuona kocha wetu akimtemea mtu mate, nina picha za video za mechi hiyo. Kwani amekua nyoka amtemee mtu mate?.''
CAF imesema itawasiliana na shirikisho linalosimamia kandanda duniani, Fifa, kuhusu uamuzi huo na huenda Fifa ikaamua kuwasiliana na wanachama wake kuhusu adhabu hiyo.
Hii inaamanisha Amrouche hatakubaliwa kufunza timu yoyote kote duniani kutokana na adhabu hiyo ya kufungiwa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment