Monday, July 20, 2015

KESI YA RAIS WA ZAMANI WA CHAD INAANZA KUSIKILIZWA

Hissène Habré azungukwa na askari baada ya kusikilizwa na jaji tarehe 2 Julai mwaka 2013 katika mji wa Dakar.
Hissène Habré azungukwa na askari baada ya kusikilizwa na jaji tarehe 2 Julai mwaka 2013 katika mji wa Daka
Na RFI
Pazia inafunguliwa leo Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar katika kesi muhimu barani Afrika ya rais wa zamani wa Chad, Hissène Habré.
Rais huyo wa zamani wa Chad, alikimbilia nchini Senegal tangu kuangushwa madarakani mwaka 1990, na anatuhumiwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na mateso.
Itakua mara ya kwanza katika historia rais wa zamani kuhukumiwa katika nchi ambayo si yake kwa uhalifu unaohusiana na haki za binadamu.
Hakuna mtu angeliweza kufikiria kwamba siku moja Hissène Habré atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kujibu matendo yake. Ili kigogo huyo wa zamani wa Chad aliye jihusisha na mabaya mengi nchini aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, ilichukua zaidi ya miaka 15 ya vita kali vya kisheria, vilioendeshwa na waathirika wakiongozana na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu, kwa njia ya kupambana dhidi ya ukatili, maamuzi kuahirishwa, hukumu juu ya rufaa,... hadi hatimaye Senegal, kwa makubaliano na Umoja wa Afrika, kuamua kuanzisha Kitengo cha Mahakama ya Afrika kilichozinduliwa mwezi Februari mwaka 2013.(P.T)
Kesi ya rais wa zamani wa Chad Hissène Habré iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu itaendeshwa katika Mahakama kuu Lat Dior, mjini Dakar kuanzia Julai 20, 2015.
" Leo hii ni ushindi wa mshikamano, uvumilivu na mawazo. Mtu mmoja kwa waathirika wa serikali hii ya kikatili ", amesema mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu, Reed Brody, huku akibaini kwamba " Jambo ambalo lilikua halifikiriwi miaka iliyopita, sasa linawezekana na hii inafungua njia kwa waathirika wengine barani Afrika na ulimwenguni ".
Uchunguzi ulidumu miezi 19. Majaji waliunda tume nne na kujielekeza nchini Chad, mashahidi na waathirika 2,500 walihojiwa na hasa kuzifanyia kazi nyaraka za za zamani za DDS, ambayo iklikua polisi wa kisiasa wa Hissène Habré.
Rais wa zamani akataa kusikilizwa na mahakama
Kwa upande wake, rais wa zamani wa Chad haitambui mahakama ambayo itamsikiliza na kumuhukumu. Hissène Habré alikua akikaa kimya wakati wa kusikilizwa, na amesema kupitia wanasheria wake kuwa amekataa kuhudhuria vikao mahakamani. "Kesi hii ni kama mchezo wa kuigiza, na ntakubali kusikilizwa iwapo wataamua kubadili mkakati, Hissène Habré hataki kuhudhuria vikao", wamearifu wanasheria wa rais wa zamani wa Chad. Katika hali yoyote, atakaa kimya. " Habré anakataa kujidhalilisha mbele ya mahakama hiyo asiyoitambua", amesema mmoja wa watetezi wake, ambaye ameshutumu kuwa " kesi ilipangwa tangu kitambo baada ya uchunguzi na Habré alituhumiwa makosa kadhaa", " hii ni dhulma dhidi ya mteja wetu", amesema mwanasheria huyo wa Hissène Habré.
Kesi hii itadumu miezi mitatu
Kulingana na sheria za Senegal, Jaji mkuu ana uwezo wa kumfikisha mahakamani kwa nguvu rais wa zamani wa Chad, hadi kufungwa pingu kama atakataa kuripoti mahakamani. Je Jaji huyu mkuu atalazimika kutumia sheria hiyo? Mpaka sasa haijajulikana kwa siku ya leo ufunguzi wa kesi ya rais huyo wa zamani wa Chad.

No comments:

Post a Comment