Monday, July 20, 2015

Shule ya Sekondari Kinyerezi Tabata jijini Dar es Salaam yanufaika na kompyuta 24 kupitia mradi wa Vodacom Foundation

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kinyerezi Tabata jijini Dar es Salaam, Judith Chalamila akiwaonesha moja ya kompyuta mpakao kati ya (24) wanafunzi wa kidato cha Nne baada ya kukabidhiwa msaada wa  kompyuta hizo zilizotolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation. Mradi huo unaoendeshwa na Learning In Sync ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo mashuleni. 
Wanafunzi wa kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya Kinyerezi Tabata jijini Dar es Salaam, John Robert na Janeth Abdallah wakimsikiliza  Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akiwafafanulia jambo kuhusiana na matumizi ya kompyuta mpakato zilizokabidhiwa na taasisi ya Vodacom Foundation ikiwa ni mradi unaoendeshwa na Learning In Sync kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo. 
Msimamizi wa Mradi wa Kompyuta mashuleni Learning In Sync, Lisa Walker (kulia)akimwelezea jambo kuhusiana na moja ya program za kompyuta Mwanafunzi wa kidato cha Nne wa shule ya sekondari ya Kinyerezi  Tabata jijini Dar es Salaam Janeth Abdallah. Wakati wa makabidhiano rasmi ya msaada wa kompyuta(24) zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation. Mradi huo ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo mashuleni. 
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Kinyerezi Tabata jijini Dar es Salaam, wakijisomea kupitia Kompyuta mpakato zilizounganishwa na kifaa cha kujifunzia masomo  mbalimbali kupitia kompyuta hizo zilizotolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Foundation. Mradi huo unaoendeshwa na Learning In Sync  ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo mashuleni.

No comments:

Post a Comment