Tuesday, July 9, 2013

DAWASCO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA KULIPIA ANKRA ZA MAJI KWA KUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI NA MITANDAO YA SIMU ZA MIKONONI

Shirika la maji safi na maji taka DAWASCO leo wamezindu njia  za mfumao wa  malipo ya  kulipia ankara za maji  kwa kutumia njia za kibenk pamoja na njia za mtandao wa simu huduma hii imezinduliwa leo katika makao makuu ya Dawasco jijini Dar es salaam.

Mfumo huu wa kulipia ankra za  ulianza tangu  tarehe 01/07/2013  katika vituo vyake 13 .mabadiliko haya  yanalenga  kuboresha huduma  kwa mteja ,pia mfumo huu utasidia  kupunguza  msongamano wa muda mrefu ulikuwepo  wa kulipia  madirishani  na utampatia  mteja njia  mbali mbali   za kulipia bili yake  kwa wakati wowote

Mfumo huu  pia utamsaidia mteja  kfanya malipo sehemu yoyote  nje ya Dar es salaam na hata nje ya Nchi.
Malipo kwa njia ya benki  yatafanyika  kwenye tawi lolote katika Benki zifuatazao :
CRDB-A/C No.01J102192190,BARCLAYS-A/C No.0014003711,BANK OF AFRICA(BOA)-A/C No.02022460009 na NMB nO.201033300047

Mteja atakwenda Benk anayotaka kufanya malipo  na kujaza  fomu ya fedha ( deposit slip) .Mteja ahakikishe ameandika namba ya account  ya Dawasco kwa usahihi ikifuatiwa  nakiasi cha fedha  anacholipa ,kisha kurudisha fomu  kwa karani wa Benki  kwa malipo.

Huduma za kibenki kwa  kutumia simu za kiganjani  ni kwa  wateja wenye account  katika Benki za :- CRDB,NMB,BENKI YA POSTA,AKIBA COMMERCIAL BANK(ACB) na EXIM BANK

Malipo kwa kutumia simu  ya kiganjani  yatafanyika kwa  kupitia M-PESA,AITEL MONEY,TIGO PESA na ZANTEL EZY PESA.
Pia waweza kulipia ankra yako kwa kupitia  ATM ZA UMOJA SWITCH, huduma ya SELCOM na MAX MALIPO inayopatikana  kwa mawakala waliopo  kila kona ya jiji la DAR ES SALAAM.

Kuna matawi ya Benk  yako karibu na vituo vya Dawasco hivyo wateja wa maeneo  husika  watapata urahisiwa kufanya malipo yao  ya kila mwezi  na kuondoa  usumbufu  wa kwenda   mbali zaidi.Matawi  hayo ya Benki  yaliyo karibu  na vituo vya Dawasco ni haya yafuatayo:-
Kituo cha DAWASCO TEMEKE kilichopo Temeke  usalama kipo  karibu na Matawi ya Benki  ya NMB Temeke Hospital  ,CRDB -Qulity  Centre.

Kituo cha DAWASCO KAWE kilichpo njia panda ya kawe  kipo karibu na  Matawi ya  Benki  ya CRDB yalipo MBEZI BEACH,KIJITONYAMA MIKOCHEN  na MLIMANI CITY  na matawi  ya NMB yaliyopo  MLIMANI CITY ,MBECHI BEACH  na MWENGE  na Tawi  la BOA BANK iliyopo  SINZA.

Kituo cha DAWASCO TABATA  kilichopo DAR WEST  kipo karibu na matawi  ya benk ya CRDB tabata magengeni.


Kituo cha DAWASCO KIMARA  kilichopo  kimara mwisho ( matankini) kipo  karibu na Matawi ya  benki  ya CRDB UBUNGO  mwisho,CRDB -Mbezi  stand mpya,CRDB-Mlimani city ,NMB,BANK OF AFRICA(BOA) zilizopo  Ubungo plaza ,CRDB Ubungo stand ,ATM ZA UMOJA SWITCH zilizopo Mbezi suka.

Kituo cha DAWASCO KINONDONI  kilichopo nyuma ya  jengo la Airtel  kipo  karibu na matawi ya Benki  ya NMB-Namanga /Msasani , ATM ZA UMOJA SWITCH -Mwnamboka ,AKIBA COMMERCIAL BANK  na CRDB  zilizopo  millenium tower  Makumbusho.

Kituo cha  DAWASCO magomen  kilichopo Magomeni Mapipa  kipo karibu na Matawi ya  Benki  ya BARCLAYS -Magomeni Mapipa  na NMB -Magomeni Mikumi.
Kituo cha Dawasco city centre  kilichopo kisutu  kipo karibu na matawi ya benki ya EXIM BANK Morogor Road  eneo la fire na CRDB -Lumumba.

kituo cha DAWASCO  ILALA kilichopo Boma jiriani na Mwalimu House ,kipo karibu na Matawi  ya Benki  ya BOA -Amana ,NMB-Boma BARCLAYS-Buguruni Malapa ,AKIBA COMMERCIAL BANK -Mtaa wa uhuru  na Likoma ,CRDB -Lumumba ,Mnzai mmoja na mtaa wa uhuru.

Kituo cha  DAWASCO  KIBAHA  kilichopo  karibu na ofisi za TRA  kipo karibu na  matawi ya benki ya NMB -Kibaha  na CRDB -Kibaha.

Kituo cha  DAWASCO Mlandizi kipo karibu na  Matawi ya CRDB na NMB.

Kituo cha DAWASCO bagamoyo  kilichopo  karibu na  ofisi  ya mkuu wa wilaya  kipo  karibu na  matawi ya Benki ya  CRDB-Bagamoyo  na NMB -BAGAMOYO

Kituo cha DAWASCO GEREZANI ( makao makuu)  kilichopo karibu na  jengo la  water front  ,kipo karibu na  na matawi  ya Benki ya  CRDB  water front ,NMB-SAMORA.

Kituo cha DAWASCO BOKO  kipo karibu  na matawi  ya NMB na CRDB jengo la  KIBO COMPLEX ,ATM ZA UMOJA SWITCH  zilizopo  eneo la AFRICANA.

LIPA BILI YAKO YA MAJI  UKIWA MAHALI POPOTE NA WAKATI WOWOTE

No comments:

Post a Comment