Na Hamida Ramadhan, Dodoma
VIJANA nchini wametakiwa kulinda mila na desturi na kuacha kuiga mambo mabaya ambayo yanachangia kuangamiza mila za Watanzania.
Ushauri huo ulitolewa hivi karibuni na Chifu Lazaro Chihoma alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Alisema vijana wengi wamesahau mila zao na kuiga mila za kigeni, jambo ambalo ni hatari kwa vizazi vijavyo. Alieleza kuwa mila ni kitu kinachoweza kumfanya kijana kuwa na maadili mema katika jamii inayomzunguka na kuachana na mambo mabaya.
“Mila na desturi kwa Watanzania zimekufa kabisa, hali inayosababisha kuvunjika kwa maadili na matokeo yake ni watoto wetu kuvaa nguo nusu uchi,” alisema Chifu Chihoma. Aliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuwalea kwa maadili mema yanayokubalika katika jamii.
No comments:
Post a Comment