Taasisi mbali mbali za kusaidia wanawake
nchini Tanzania wametakiwa kujitangaza kwa jamii na kwa kwa wananwake wenyewe
ili wanawake waweze kuzifaham na kutumia fursa zinazotolewa na taasisi hizo
katika kuinua maendeleo kwa kupitia kundi la wanawake wanaojiunga katika jamii ili kujikomboa
kiuchumi.
Hayo yamesemwa na askofu mkuu wa kkkt
dayosis ya Mashariki na pwani na makamu
wa rais wa muungano wa makanisa ya kiluther duniani Dr Alex Malasusa alipohudhuria mkutano wa
majadiliano wa kusaidia wanawake kwa
kuwawezesha mambo ya kifedha ili kuweza kuinua uchimi nchini Tanzania .
Amezidi kuwaomba wanawake kutumia taasis za
kusaidia wanawake na hasa amewaomba
wanawake kuwa waaminifu katika kurudisha mikopo waliyopewa ili kuwezesha
taasisi hizo kuweza kuwasaidia wanawake wengi kuweza kujikwamua na umasikini na
kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake mwanzilishi wa taasisi
ya kutoa mikopo na kuwa saidia wananwake
katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo iitwayo SELFINA ,DR VICTORIA KISYOMBE amesema kama Watanzania
wanataka kupata maendeleo ni lazima wapige vita Rushwa ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo.
Akifafanua jinsi rushwa inavyorudisha
maendeleo Dr kysombe na mwanzilishi wa taasis ya Selfina ,amesema rushwa ni
adui mkibwa wa maendeleo ,hivyo kuwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika
kupiga vita rushwa ili kupatikana kwa
usawa katika upatikanaji wa mikopo kwa
wanawake ambapo pia ameishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa
kupigana vilivyo na tatizo la rushwa hapa nchini.
Pia ameshukuru kuwa dunia inatambua umuhimu
wa kusaidia wanawake ili wanawake waweze kujikomboa kiuchumi pamoja na haya pia
ameshukuru mabenki ambayo yametambua umuhimu wa kuwasaidia wanawake kwa kuwapa
mikopo.
Katika hayo pia amesema changamoto kubwa
inayowakabili tasisi nyingi ni ukosefu wa matawi ya benk vijijini kwani makampuni mengi ya kibenki yamejiwekeza
zaidi katika miji mikubwa na kusau
kujiwekeza vijijini na kutoa wito kwa makampuni ya kibenki kushirikiana na Taasisi ya Selfina
katika kutoa mikopo ya bei nafuu kwa
wana wake ili kuweza kuwasaidia wananwake wa mjini na vijijini kuinuka katika
suala la kimaendeleo na kiuchumi.
No comments:
Post a Comment