Jeshi la Burma linasema kuwa mabaki yamepatikana baada ya ndege ya jeshi kutoweka ikiwa na watu 122.
Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na jeshi.
Ndege hiyo aina ya Y8 iliyotengezwa nchini China ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.
Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano
Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.
Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi walifariki wakati ndege hiyo ilianguka kwenye mji mku wa Nay Pyi Taw.
Miezi mitatu baadaye maafisa watatu waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilianguka kati kati mwa Mynmar.
No comments:
Post a Comment