Monday, July 20, 2015

Balozi Seif Idd afungua Tamasha la 18 la Filamu la nchi za Jahazi (Ziff) Mjini Zanzibar

Baadhi ya washirika wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF), waliohudhuria uzindazi wake kutimia miaka 18 tokea kuasisiwa kwa Tamasha hilo hapa Nchini.  
Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger akiahidi taasisi yake kuendelea kusaidia vipaji vya vijana katika utengenezaji wa filam zilizo bora Nchini.
Mkurugenzi wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar   (ZIFF) Profesa Martin Mhando akitoa neneo la makaribisho kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo hapo shangani. 
Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF) hapo Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar. 
Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF) hapo Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wa Pili kutoka Kushoto akiwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein akijumuika pamoja na baadhi ya viongozi kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar hapo Double Tree By Hilton Shangani mjini Zanzibar leo. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mhmoud Thabit Kombo na msanii wa filam ya sarafina kutoka Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF), Mahmoud Thabit Kombo akitoa neon la kumkaribisha mgeni rasmi kulizindua Tamasha hilo hapo Double Tree By Hilton Shangani. 
Msanii Mkongwe wa nyimbo kutoka Johannesburg Nchini Afrika Kusini  Doroth Masuka akipongeza juhudi zinazochukuliwa  na Serikali pamoja na washirika wake katika kuimarisha vipaji vya wasanii hapa Nchini.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi  na washirika wa Tamasha la Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya kulizindua Tamasha hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Kulia kwa Balozi Seif Idd ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michiezo Mh, Said Ali Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia, kukuza vipaji vya wasanii katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ZUKU) Bibi Maud Roger. Kushoto kwa Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF) Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Msanii Maarufu Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka nchini Afrika Kusini, Bibi Laleta Kumalo. 
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi  na washirika wa Tamasha la Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya kulizindua Tamasha hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Kulia kwa Balozi Seif Idd ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michiezo Mh, Said Ali Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia, kukuza vipaji vya wasanii katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ZUKU) Bibi Maud Roger.  Kushoto kwa Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar (ZIFF) Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Msanii Maarufu Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka nchini Afrika Kusini, Bibi Laleta Kumalo. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)

Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/7/2015.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono  juhudi zinazochukuliwa na Uongizi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi  Zanzibar { ZIFF } katika azma yake ya kuijengea nguvu tasnia ya Filam Nchini inayoonekana kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya Utalii.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati  akilizindua Tamasha la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.

Dr. Shein  alisema kwamba Tamasha la Nchi za jahazi limekuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza Zanzibar Kimataifa hali ambayo imetoa ushawishi kwa wageni na watalii wengi kuamua kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar kujionea mazingira na rasilmali zilizopo.

Alisema kupitia Tasnia ya filam zinazotayarishwa na wasanii mbali mbali kwa kushirikiana na wadau wa Fani hiyo chini ya Wataalamu wa Ziff wageni na watalii mbali mbali Duniani wamekuwa wakivutiwa na fukwe pamoja na Utamaduni  uliojaa ukarimu wa Watu wa Visiwa vya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } kuendelea kufanya juhudi zaidi za kuwashawishi wasanii wa Kimataifa kuzitumia Fukwe na Tamaduni za Zanzibar katika kutengeneza Filam mbali mbali kwa lengo la kuitangaza zaidi Zanzibar Kimataifa.

“ Zanzibar  ni Visiwa vya maumbile ya Utamaduni ya Ukarimu pamoja na fukwe za kuvutia mambo ambayo yakitangazwa vyema wasanii wa Kimataifa wanaweza kushawishika kuyatumia katika kutengeneza Filamu zao “. Alifafanua Dr. Shein.

Alifahamisha kwamba Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi, Tamasha la Iddi, Tamasha la Mzanzibari pamoja na  Sherehe za Mwaka Kogwa zinazofanyika Makunduchi ni Mambo muhimu yanayopaswa kuimarishwa katika kukuza na kusimamia Utamaduni na Historia ya Zanzibar na Watu wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewapongeza Wasanii wa Maigizo pamoja na Filam Nchini  kutokana na kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kuelimisha Jamii sambamba na kuwapatia Burdani.

Alisema mbali ya Tasnia hiyo kutoa ajira pana kwa kundi kubwa hasa Vijana Nchini lakini pia imepanua soko la filam za nyumbani na kuleta unafuu kwa kila mtu kumudu kununua na kuangalia kazi za wasanii wa hapa Nchini hali iliyopelekea kufikia asilimi 80% ya filamu za Kiswahili zinazoangaliwa tofauti na miaka iliyopita nyuma.

Mapema Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger aliahidi kwamba Taasisi yake itaendelea kukuza vipaji vya wasanii kwa lengo la kufikia kiwango kinachokubalika Kimataifa.

Bibi Roger alisema hatua hiyo muhimu itaweza kuwajengea uwezo wa kiajira badala ya kusubiri kutegemea zile za Serikali ambazo kwa sasa upo upungufu mkubwa hata katika Mataifa yaliyoendelea.

Meneja wa Taasisi hiyo ya Zuku alifahamisha kwamba mpango maalum umeandaliwa na Uongozi wa Taasisi hiyo baina ya miaka sita na kumi kwa kuwadhamini Vijana wapatao Kumi wanaopata Mafunzo ya msingi kuweza kutengeneza Filam zitazokubalika Kimataifa.

Wakitoa salamu zao kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi Msanii Gwiji  Duniani kutoka Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo aliyeigiza filam Maarufu ya sarafina pamoja na Msanii Mkongwe wa Nchi Hiyo Doroth Masuka wameelezea faraja yao kutokana na Serikali kupitia taasisi za kijamii zilivyojikita katika kusaidia vijana kwenye fani ya sanaa.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la 18 la Ziff Mwenyekiti wa Bondi ya Tamasha hilo Mahmoud Thabit Kombo alisema Ziff itaendelea kushirikiana na wadau wote wa ndani na nje ya nchi katika kuona Taasisi hiyo muhimu inazidi kuimarika.

Mahmoud Thabit Kombo alisema uimarikaji huo utawapa nguvu na ari Vijana walioamua kujiajiri kupitia Tasnia ya Filam inayoonekana kupata umaarufu siku hadi siku hapa Duniani.

Uzinduzi wa Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi  za Jahazi Zanzibar (ZIFF) limekwenda sambamba na siku yake lililoasisiwa rasmi Tarehe 18 Julai Mwaka 1997 likitimiza umri wa miaka 18 sasa.

No comments:

Post a Comment