Tuesday, August 12, 2014

POLISI SENGEREMA WAKAMATA ZAIDI YA TANI 2 ZA SAMAKI WALOVULIWA KIHARAMIA.

Ni samaki zaidi ya tani 2 wasiokuwa na viwango halali vya kuvuliwa wamekamatwa leo asubuhi katika mwalo wa kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya zoezi la kuwakamata wavuvi haramu kufanyika ziwani Victoria.
Zoezi la msako kwa wavuvi haramu ziwani victoria hususani katika kijiji cha Katunguru linaendeshwa na Kikundi cha B.M.U cha Juma Kisiwani kwa ushirikiano na jeshi la Polisi wilayani Sengerema na hapa pichani askari polisi wakichukuwa vielelezo toka kwa mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa wakimiliki samaki hao.

Samaki hawa wamevuliwa na nyavu ndogo zilizopigwa marufuku katika uvuvi ziwa Victoria. 
MKUU wa Jeshi la Polisi wilaya ya Sengerema CP Adre Yohana ametoa wito kwa jamii kuacha kabisa kutumia nyavu ndogo zilizopigwa marufuku au kutumia mifumo ya uvuvi kwa kutumia sumu kwani kufanya hivyo ni kupoteza jamii ya viumbe samaki ambao ni muhimu katika uchumi wa watu wa ukanda wa ziwa Victoria.

Amesema kuwa wakati umefika kwa jamii kuheshimu sheria zilizopo zikiwemo za uvuvi na uhifadhi wa mazingira ili matumizi ya rasilimali za ziwa na mali asili ziwe endelevu kwa maslahi ya wananchi na vizazi vijavyo.

Katika hatua nyingine wadau wa udhibiti wa uvuvi haramu wa Kikundi cha B.M.U cha Juma Kisiwani wamesema kuwa jamii inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo umasikini, ukosefu wa elimu juu ya uvuvi wa kisasa wa zao la samaki sambamba na kutoona umuhimu wa kutunza mazalia ya samaki na viumbe wengine majini.
Wananchi wakiwa eneo la tukio kushuhudia zoezi hilo la ukamataji wavuvi haramu pamoja na samaki walio vuliwa chini ya viwango.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO BLOG.

No comments:

Post a Comment