Monday, August 11, 2014

MAFUNDI GEREJI TEGETA WAZO HILL WATAKIWA KUHAMA HARAKA

#UMOJA WA MAFUNDI GEREJI  KATIKA ENEO LA  TEGETA  WATAKIWA KUHAMA MARA MOJA KUTEKELEZA  AMRI YA MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI#

Serikali imewataka wananchi wanaojulikana kama UMOJA WA MAFUNDI kuhama mara moja  kutoka katika eneo la Tegeta Wazo Hill na kuhamia katika eneo la NYAKASANGWE  katika kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam,Kabla ya tarehe 17/08/2014 ili kutekeleza amari ya mahakama kuu kitengo cha Ardhi.

Kauli hiyo imetolewa na  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Sadick Meck Sadiki  alipokuwa katika eneo la NYAKASANGWE ,Lilipotengwa kuwa eneo jipya lilotengwa kwa ajili ya umoja huo ,akiwa maeongozana na kamati ya Ulinzi na Usalama.

Aidha ametoa  siku tatu kuanzia leo tarehe 11/08/2014 hadi tarehe 13/08/2014  mafundi hao wawe wamekwisha ondoka katika eneo hilo, na wametakiwa  kuhakikisha kuwa wanafika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kinondoni kuanzia jana kwa lengo la kujiandikisha na pia kupata taratibu zingine zinazohusu eneo hilo jipya zilizoandaliwa .

Umoja huo umekuwa ukifungua kesi mahakamkani mara kwa mara kudai uhalali wa eneo hilo lakini mnamo tarehe 18/07/2014 mahakama kuu kitengo cha ardhi  ilitoa amri kuwa watu hao wahame katika eneo hilo kabla ya kufika tarehe 17/08/2014.

Kwa Busara ya uongozi wa mkuu wa mkoa Dar es salaam ulimwomba mwekezaji anayetambulika kama NYANZA ROAD WORKS kuwasadia ili waweze kupata eneo lingine ndipo ,Mwekezaji huyo alipotoa eneo lake  lenye ukubwa wa hekari 37  Lilopo  eneo la NYAKASANGWE  katika kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam ili waweze kugawia na kuendelea na shuguli zao  za kuwapatia kipato kutokana na  taratibu zilizowekwa.

Mkuu wa mkoa ametoa onyo kali kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya kuhama kutoka katika eneo hilo la Tegeta kuwa atachukuliwa hatua kali za kinidhamu  ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakani ili kujibu tuhuma za  kukaidi amri   hiyo ya Kuhama.

No comments:

Post a Comment