Umoja wa Ulaya umevitaka vyombo vinavyohusika na ubora wa chakula kuifanyia vipimo vya vinasaba nyama inayouzwa katika nchi za Umoja huo, ili kurejesha imani ya watumiaji kufuatia kashfa ya nyama ya farasi madukani.
Vipimo hivyo vitatoa uhakika kama kweli hiyo ni nyama ya mifugo iliyoandikwa kwenye masanduku yake. Wakati huo huo, uchunguzi umeanza nchini Ujerumani, baada ya serikali kuamuru kutupwa kwa kiasi kikubwa cha nyama ambayo ilidhaniwa kimakosa kuwa nyama ya farasi.
Nchini Uingereza, watu watatu wamekamatwa kuhusiana na kashfa hiyo ya kuuza nyama ya farasi. Wawili kati yao walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda cha kusindika nyama huko Wales, na mwingine ni mfanyakazi wa machinjioni katika eneo la West Yorkshire. Waziri wa mazingira wa Uingereza Owen Paterson amesema ngazi za sheria zinaiangalia kashfa hii.
Ufaransa imeifutia leseni kampuni ya Spanghero ambayo imehusishwa na kashfa hiyo. Kampuni hiyo inashutumiwa kuuza tani za nyama ya farasi, ambayo kwa makusudi iliwekewa alama ya nyama ya ng'ombe
habari na dw swahili
No comments:
Post a Comment