Familia ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius 
anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji, imesema inapinga vikali 
tuhuma kwamba amemuuwa mpenzi wake. Tangazo lililotolewa na 
familia hiyo vile vile limetoa salamu za rambirambi kwa familia ya 
msichana aliyeuawa, Reeva Steenkamp.
Oscar Pistorius amefunguliwa rasmi mashitaka ya kumuuwa mpenzi wake asubuhi ya leo. Baada kusomewa mashtaka hayo, Pistorius mwenye umri wa miaka 26 aliangua kilio na kububujikwa na machozi mahakamani.
Mwanariadha huyo anayekimbia kutumia miguu ya bandia, anatuhumiwa kumpiga risasi nne na kumuua mpenzi wake, katika nyumba yake iliyo kwenye mtaa wa matajiri mjini Pretoria.
Polisi walitupilia mbali madai ya awali kwamba mwanariadha huyo alimfyatulia risasi mpenzi wake kimakosa, akidhani ni mwizi. Gazeti la Beeld ambalo ndilo la kwanza kutangaza kisa cha mauaji hayo, limesema kuwa Pistorius alimpiga risasi Reeva Steen-kamp kupitia mlango wa bafu lake.
habari na dw swahili

No comments:
Post a Comment