Friday, February 15, 2013

Korti kuu ya Kenya: Uhuru na Ruto wako huru kugombea

Mahakama Kuu ya Kenya imesema haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi dhidi ya mgombea wa urais, Uhuru Kenyatta na na mgombea mwenza wake William Ruto. Kesi kuhusu suala hilo iliyokuwa imefunguliwa na vyama vya kiraia sasa inahamishiwa kwenye Mahakama ya Juu.
Kesi hiyo ilifunguliwa kupinga ushiriki wa watu hao katika uchaguzi wa mwezi Machi, kwa kile walichokiita kukosa uadilifu kwa sababu tayari wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC.
Kenyatta ambaye ni mwanae rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, na William Ruto ni miongoni mwa watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa na ICC kuchochea ghasia hizo za baada ya uchaguzi, ambamo watu zaidi ya 1200 walipoteza maisha.

No comments:

Post a Comment