Friday, February 15, 2013

Mripuko wa vimondo wajeruhi 700 Urusi


Maafisa nchini Urusi wamesema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa na mripuko wa kimondo imepanda na kufikia 700, miongoni mwao wakiwemo watoto 159. Mripuko huo umetokea katika eneo la Chelyabinsk katika milima ya Urali. Mapaa ya nyumba katika miji sita yameharibiwa na vioo vya madirisha vimevunjwa.

Eneo la Chelyabinsk lililokumbwa na mkasa huo liko umbali wa kilomita 1,500 kutoka mji mkuu Moscow. Vimondo ni vipande vinavyomegeka kwenye sayari ndogo zinazozunguka angani.

Wakati huo, usiku wa leo, sayari ndogo itaikosakosa dunia kwa umbali wa kilomita 27,000. Sayari hiyo iliyopewa jina la 2012 DA 14 ina kipenyo cha mita 68, na uzito wa tani laki nne itapita karibu na dunia saa nne na dakika ishirini na tano kwa saa za Afrika Mashariki, hii ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la anga la Ulaya, ESA.

Afisa wa shirika la anga la Marekano, NASA, Donald Yeomans amesema hawana wasiwasi juu ya sayari hiyo. Hakuna uhusiano kati ya sayari hiyo na vimondo vilivyoripuka nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment