Wanajeshi watano wa Uganda waliyokuwa kwenye helikopta
zilizoanguka nchini Kenya wameokolewa wakiwa hai huku wawili
wakithibitika kufariki. Mhifadhi mwandamizi kutoka shirika la huduma
za wanyamapori, KWS,
Simon Gitau amesema wanajeshi hao watano walikuwa na afya njema na walipelekwa na ndege katika eneo salama. Helikopta tatu za kijeshi aina ya Mi-245 zilizotengenezwa nchini Urusi zilianguka katika eneo lilijitenga nchini Kenya wakati zikielekea nchini Somalia kutoa msaada kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika.
Moja ya helikopta hizo ilipatikana siku ya Jumatatu na wanajeshi wote saba waliyokuwemo waliokolewa. Mabaki ya helikopta mbili yamepatika leo asubuhi ambapo miili ya wanajeshi wawili ilionekana katika moja iliyokuwa inawaka moto, alisema Gitau. Mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Kenya Jenerali Julius Karangi aliwambia waandishi wa habari kuwa helikopta moja ilikutwa imeungua kabisaa na nyingine ilikuwa ikining'inia kwenye mteremko wa mlima.
Awali iliripotiwa kuwa helikopta zote mbili zilikuwa zimeungua baada ya kuanguka. Jumla ya maafisa 14 walikuwemo katika helikopta zote mbili na hii inamaanisha kuwa maafisa wengine saba bado hawajajulikana waliko .

No comments:
Post a Comment