| ||||
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. |
…………………………………………………………………………………………………………
Kampuni
ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji vyenye thamani ya
174m/- kwa vijiji 12 mkoani Singida ikiwa ni kuchangia juhudi za
serikali za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.Akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko
wilayani Singida mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini
George Lugata alisema ufadhili huo umo kwenye mikakati ya kampuni ya
kusaidia jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
Vijiji
vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye
mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba),
Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na Damankia (Ikungi).
Vingine ni Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni),
Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda
(Kinampanda).
“Msaada
huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii ambayo
inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi,
Tigo inasaidia kutatua uhaba mkubwa wa maji katika eneo hili la mkoa
wa Singida ambalo kwa kiwango kikubwa limekumbwa na uhaba mkubwa wa
mvua katika kipindi cha miaka mine iliyopita,” alisema Lugata.
Aidha
aliongeza kuwa uhaba wa maji miongoni mwa wilaya nyingi za Singida
umesababisha wakiazi wake kupoteza muda mwinmgi kutafuta bidhaa hiyo
muhimu, jambo ambalo Tigo inaamini kuwa hivi sasa litafikia ukomo
kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
Makabidhiano
ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye aliishukuru Tigo kwa
ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo
vitapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba sugu wa maji uliolikumba eneo
hilo na kuchangia kukua ustawi wa jamii kijamii na kiuchumi.
Hata
hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia kwenye
juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa
Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua uhaba wa maji
uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima
hivi 12 vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili
linaloikabili jamii kwa sasa”.
No comments:
Post a Comment