Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya
nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar
es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni
mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
tangu mwaka 2012.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza
katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na
Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako
Mwakalobo.
Ofisa
Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano
huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza
na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za
Kanda, Terry Edward.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
BOHARI
ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa
njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili tangu mwaka 2012.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka
2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.
Bwanakunu
alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani
ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.
"Tunapenda
kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini
hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali
ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.
Alisema
kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa
imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na
vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo
ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.
Aliongeza
kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na
vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka
na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya
kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.
Akitolea
ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari
aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD
amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.
Katika
ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo
havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya
sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki
moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment