MKUU
wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala akizungumza
wakati wa kuhitisha mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la
Misaada la Marekani (USAID) na kutekelezwa katika Halmashauri 97 katika
mikoa 13 nchini. Uzinduzi wa mradi wa PS3 ngazi ya mkloa wa Mtwara
ilifanyika juzi mjini humo.
Mkoani
Mtwara mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
itahusisha Halamshauri ya Nanyamba na Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Awamu ya pili ambayo itatekelezwa
mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na
Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji
wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya
yaTandahimba.
Baadhi
ya Maofisa wa Mradi wa PS3 pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya Mkoani Mtwara wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Rasilimali Fedha, Dk Daniel Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mshauri
wa Mradi katika Masuala ya Elimu, Dk Rest Laswai akifafanua jambo juu
ya uimarishaji mifumo ya sekta za Umma katika nyanja ya elimu.
Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Maafisa wa Mradi wa PS3 Godfrey Nyombi (kulia) na Rahma Musoke wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya vikundi.
Mtaalam wa Fedha wa Mradi wa PS3, Abdul Kitula akifafanua jambo katika moja ya vikundi vilivyokuwa katika majadiliano.Dk Rest Laswai (kushoto) akisimamia majadiliano ya moja ya vikundi.
Makundi mbalimbali yakishiriki katika majadiliano na baade kuwasilisha taarifa za mijadala yao.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment