Kesi
ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa
ubunge jimbo la Ndanda wilaya ya Masasi,Mariam Kasembe (CCM)dhidi ya
Mbunge wa jimbo hilo, Cecil Mwambe (Chadema) imeendelea kusikulizwa leo
baada ya kuahirishwa jana na Jaji Winfrida Kosoro ambapo pia leo
imepigwa tarehe hadi ijumaa ya wiki hii ambapo ndiyo mahakama itaamua
kama mshtakiwa atakuwa na kesi ya kujibu.
...Kesi
hiyo iliendelea kusikilizwa hapo jana na upande wa mdaiwa kutoa
ushahidi baada ya mleta maombi kupeleka mashahidi wiki iliyopita ambapo
wakili wa mjibu maombi, Tundu Lissu aliieleza mahakama kuwa ushahidi
uliotolewa na upande wa mpeleka maombi unapaswa kuangaliwa kwa makini
kwasababu hakuna ushahidi wowote wa nyaraka.
Pichani
ni wananchi wa jimbo la ndanda wakiwa mahakama ya wilaya masasi
kusikiliza kesi ya kupinga matkeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea
ubunge wa jimbo hilo MARIAM KASEMBE wa CCM dhidi ya mbunge wa jimbo
hilo CECIL MWAMBE wa CHADEMA
No comments:
Post a Comment