kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo |
Na Woinde Shizza,Arusha
Kufuatia zoezi la kuhakiki silaha linaloendelea hapa nchini jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa
kuhakiki jumla ya silaha 2640 na jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa
zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .
Akiongelea
swala hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa
silaha silaha hizo zimebaki chini ya
uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya
wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha
,wengine wakiwa wagonjwa pamoja
na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha
hizo.
Alisema kuwa
umri wa kumiliki silaha mwisho ni miaka 70
ambapo kuna baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanamiliki silaha hizo
tayari wameshafikia ukomo wa umri wa kumiliki silaha hizo kisheria.
Aidha
alisema pia kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanamiliki silaha zaidi ya moja
bila sababu yeyote nao wamenyang’anywa huku wengine wakiwa wamechukuwa silaha
hizo bila kujua matumizi halali ya umiliki wa silaha hizo.
Alitaja aina
ya silaha ya silaha mbalimbali ambazo tayari
zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.
Alisema kuwa
jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao
wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi
likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa
nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha
sheria .
Mkumbo pia
aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza
kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi
arudi kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi
juu ya matumizi sahihi ya silaha.
No comments:
Post a Comment