Tuesday, October 25, 2016

BALOZI MAHIGA AWAASA VIJANA NCHINI KUCHANGAMKIE FURSA ZA AJIRA ZINAZOPATIKANA UMOJA WA MATAIFA (UN)

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema ushirikiano wa Tanzania na umoja wa mataifa (UN) wataendeleza ulinzi wa amani katika mataifa mbalimbali kama wanavofanya kwa Sudan ya kusini. 
Akizungumza katika hafla ya miaka 71 ya umoja huo Dar es salaam , Balozi Mahiga amewataka Vijana nchini kuchangamkie fursa za ajira zinazopatikana umoja huo.hafla za miaka 71 za umoja wa mataifa zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa huku suala la ulinzi ' pamoja na amani likiwa limepewa kipaumbele kwa mataifa 
Naye Mwakilishi wa Mashirika wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amezitaja changamoto zinazoikabili UN ni ongezeko la vijana ambapo wengi huwa wanashindwa kuendana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kutokana na miundombinu ya Elimu kutokuwa Rafiki. 
Rodriguez ameongeza kuwa Ili kuhakikisha UN inakabiliana na Changamoto hiyo wameweka nguvu zaidi katika kuboresha Miundombinu ya Elimu barani Afrika ili vijana kuweza kuendana na kasi ya utandawazi ili kuweza kujiajiri. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga akizungumza kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja wa mataifa (UN) jana jinini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja mataifa (UN) jana jinini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment