Wednesday, October 19, 2016

MREMBO WA SINZA, SIA PIUS AWA TOP MODEL WA MISS TANZANIA 2016


Washiriki wa Miss Tanzania 2016 kutoka Kanda ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa katika pozi.
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 kutoka Kanda ya Mashariki wakiwa katika pozi. 
Juu na chini: Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha ya pamoja ziwani Singida.

Na Mwandishi wetu, Arusha
SHINDANO dogo la kumtafuta mrembo mwanamitindo TOP MODEL limefanyika  mkoani Arusha Jumamosi iliyopita huku mrembo wa Sinza Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni akiibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.

Jumla ya warembo 30 walipanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo ni la pili kushindaniwa kati  ya Mataji 5 yanayo shindaniwa  kabla  ya shindano kubwa la Fainali za Miss Tanzania lililopangwa kufanyika jijini Mwanza tarehe 29 Oktoba 2016.

Washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameingia kambini tangu tarehe 30 Septemba 2016 jijini D’salaam , na baadae kuanza ziara rasmi ya kutembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na kumaliza ziara yao jijini Mwanza.

Wakiwa Makao Makuu ya Chama na Serikali mkoani Dodoma  warembo hao 30 walishiriki katika shindano dogo la kumtafuta mrembo anaevutia katika picha. (Miss Photogenic) ambapo mrembo wa Dodoma Anna Nitwa aliibuka mshindi   katika shindano hilo akifuatiwa na Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni.

Washindi hao 2 Miss Photogenic  Anna Nitwa na Top Model Sia Pius tayari  wamejipatia tiketi ya kuingia katika hatua ya pili ya nusu Fainali (Top 15) huku mataji mengine 3 bado yanagombaniwa na washiriki hao 30.

Mashindano hayo madogo yaliyobaki ni

Mrembo mwenye kipaji – Miss Talent

Mrembo mwanamichezo -  Top sports woman

Mrembo chaguo la watu – Miss Personality


Mataji hayo  madogo  yote  yatashindaniwa jijini Mwanza wiki hii kabla ya Fainali za Taifa zilizopangwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2016. Katika ukumbi wa Rock City Mall uliopo jijini Mwanza. 

No comments:

Post a Comment