Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi
Stella Manyanya (kulia), akihutubia wakati alipokuwa akifungua kongamano
la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam jana.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi
Stella Manyanya (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipokuwa amewasili kwenye kongamano la
maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika chuoni
hapo Dar es Salaam jana. Kushoto ni mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack
Mwakalila. Manyanya alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo.
Mgeni
rasmi wa kongamano hilo Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kulia
waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
walioshiriki kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto niMwanasiasa Wilson Mkama akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Mwenyekiti wa kongamano hilo, Spika wa Bunge mstaafu, Anna Makinda akizungumza kwenye kongamano hilo.
wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mkuu
wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila,
akizungumza kwenye kongamano hilo. Kongamano hilo liliandaliwa na chuo
hicho.
Waalikwa wakisikiliza wakati mada zikiendelea kutolewa.
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philipo Mangula,amesema ameanza
kupokea mafaili ya wana CCM ambao wameanza kujipitisha kutoa rushwa kwa ajili
ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho unaotajariwa kufanyika mapema mwakani.
Mangula
amesema ana taarifa kwamba wanaCCM wengi wameanza kutumia mbinu
chafu za fedha kutaka nafasi mbalimbali na kwamba imekulakwao kwakuwa
hawataweza kupenya atawashughulikia.
Mangula
alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mada ya maadili ya viongozi kwenye kongamano
la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chu
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam jana na
kueleza kukerwa na tabiya ya wafanyabishara wenye fedha ya kutaka kuteka kila
mahali.
Alisema
ndani ya CCM nimaarufu kwa jina la mzee wamafaili, hivyo ataendelea kupitia
mafaili hayo ilikuhakikisha maadili yanazingatiwa na kuenzi misingi yaAzimio la
Arusha kwani hakuna atakayepenya kwa njia za rushwa.
“Zipo
taarifa kuwa wapo baadhi wameanza kujipitisha na kutoa rushwa kwa ajili ya
uchaguzi wa mwakani, nawahakikishia kwangu watu hao hawawezi kupitani
tamfuatilia kila mmoja atakaye jihusisha na rushwa hapati nafasi hiyo,” alisema.
Alisema
ili kudhibiti mianya hiyo atahakikisha sheria inatungwa ya kutenganisha kati
ya wafanyabiashara na uongozi kwa vile wafanyabishara wanatafuta nafasi
ya uongozi ilikuendeleza biashara zao.
Mangula
alisema ni aibu kwa mpiga kura kuhongwa kiasi kidogo cha pesa na kupoteza haki
ya msingi ya kumchangua kiongozi mwenye sifa kwa ajili ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment