Na Greyson Mwase, Lindi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amewataka
watumishi wanaofanya kazi katika kituo cha cha kupokea gesi kutoka
Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha
Somanga Fungu, kutunza mitambo na miundombinu ya mabomba ya kusafirisha
gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuepuka gharama za
matengenezo ya mara kwa mara.
Profesa
Ntalikwa alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa kituo
hicho katika ziara yake ya kukagua miundombinu ya gesi katika mikoa ya
Lindi na Mtwara.
Alisema
kuwa mitambo na miundombinu ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam kupitia Lindi na Pwani, inahitaji umakini wa hali ya juu
katika uendeshaji wake pamoja na utunzaji ili mradi uwe na manufaa.
Alisema
wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanahitaji nishati ya umeme
ya uhakika na kulitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha
linaweka mikakati ya kuhakikisha gesi inayozalishwa inatumika ipasavyo
katika uzalishaji wa umeme.
“
Kutokana na kuwepo kwa nishati ya uhakika ya gesi, Tanesco mjipange
kuitumia gesi hiyo kwenye mitambo yenu na kuhakikisha kuwa baadhi ya
maeneo ya Lindi yanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme,” alisema
Profesa Ntalikwa.
Mtaalam
kutoka kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya
kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, Mhandisi Kelvin
Kasian (kulia) akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) mabomba ya gesi katika kituo hicho.
(hayapo pichani).
Mabomba
ya kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa
kwenda Dar es Salaam katika kituo cha Somaga Fungu kama yanavyoonekana
pichani.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi
Kapuulya Msomba (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (katikati) katika kituo
cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa
kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi
Kapuulya Msomba (kulia) akielezea matumizi ya chumba cha kuhifadhia
nyaraka Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin
Ntalikwa (kushoto) katika kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na
Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu.
Mtaalam
kutoka kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya
kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, Mhandisi Kelvin
Kasian (kulia mbele) akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto mbele) kwenye ziara katika
kituo hicho.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC) Dk. Shufaa Al-beity akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akielezea
mikakati ya serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya
uhakika ya umeme katika kikao chake na wafanyakazi wa kituo cha kupokea
gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es
Salaam cha Somanga Fungu (hawapo pichani)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kupokea gesi
kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam
cha Somanga Fungu
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (wa nne
kutoka kulia, waliosimama mbele) Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. Shufaa Al-beity ( wa
tano kutoka kulia, waliosimama mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba ( wa sita
kutoka kulia, waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara alipofanya ziara
kwenye ofisi hizo.
No comments:
Post a Comment