Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba,
(kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service,
Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme
(transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya
TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia
mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa
KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika
la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za
Kimarekani
309.26
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha
Tanzania na Kenya.
Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali, limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
“
Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
“Dola za Marekani Milioni 258.82,
zitatumika kujenga upande wa Tanzania na Dola za Kimarekani Milioni
50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi
Mramba. Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo kwa wakandarasi waliopewa kazi hiyo
kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba. “Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo
tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO hatutakubaliana na hilo.”Alionya Mhandisi Mramba.
Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika. Kwa upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues
Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba
Mhandisi
Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera
Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza
Mhandisi
Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum
Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bi.
Rosina wa JICA
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mratibu
wa Miradi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi
Khalid James, (kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na
Mwakilishi mkazi wa AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha
ya pamoja na wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa
mradi huo
Kutoka
kushoto, Patrick Canton, S.K. Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba,
Tonia Kandiero na Bisera Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja
mwishoni mwa hafla hiyo
Afisa
Mawasiliano na Uhusiano wa TANESCO, Henry Kilasila, (kualia),
akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Felchesmi Mramba.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU
No comments:
Post a Comment