Kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 14 ameuwawa leo
kwenye mashambulizi ya angali ya jeshi la Israel karibu na mji wa
Gaza.
Kwa mujibu wa duru za hospitali, idadi ya Wapalestina waliouwawa katika siku tatu za machafuko sasa imeongezeka na kufikia wanane. Moalem al-Adam ameuwawa wakati kombora lilipoanguka katika shamba moja katika kitongoji cha Zeitun, mashariki mwa Gaza.
Babake amejeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo. Hadi sasa jeshi la Israel halijasema lolote. Hapo awali mwanamgambo wa chama cha Hamas, Ghaleb Ermilat, aliuwawa kwenye mashambulizi mengine ya angani ya jeshi la Israel.
Israel inasema Ermilat alikuwa gaidi wa kimataifa aliyehusika na mashambulizi katika eneo la mpakani kati ya Israel na Misri, yaliyomuua Muisraeli mmoja mapema wiki hii.

No comments:
Post a Comment