Monday, January 21, 2013

PICHA ZA TUKIO LA KUANGUKA KWA UKUTA KATIKA KITUO CHA MABASI UBUNGO NA KUHARIBU MAGARI.



 
Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
 
Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.
 
Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.
Gari aina ya Toyota Saloon ikiwa imebamizwa vibaya
Hivi ndivyo ilivyokuwa
 
Baadhi ya watu wakiangalia magari yao.
Kenyela akiongea jambo juu ya ajali hiyo.
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri  umeanguka na kuyaharibu vibaya magari  zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.

                                Source: Global Publishers                         
                               Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

No comments:

Post a Comment