Monday, February 3, 2014

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam yasaidia waathirika wa Mafuriko mkoani Morogoro


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wilayani Kilosa kwa ajili ya wananchi wa mkoa huo, waliokumbwa na mafuriko hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Gharib Said Mohammed, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali, vikiwemo mabati, vyakula, nguo, vyombo vya nyumbani pamoja na vifaa vya Shule. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Gharib Said Mohammed (kulia), kutokana na misaada aliyoitoa kwa waathirika wa mafuriko mkoani humo, wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ilipofika kutoa misaada kwa waathirika hao, mwishoni mwa wiki. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova na katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko, mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Kamati hiyo, ilikabidhi msaada wa jumla ya sh. milioni 117.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki (kushoto), akizungumza, wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, ilipokuwa ikikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali, nguo, mabati, magodoro, vyombo vya nyumbani, sabuni na vifaa vya Shule kwa wananchi wa Morogoro, waliokumbwa na mafuriko hivi karibuni, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 117, mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa huo, Joel Bendera na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua habari, wakati wa makabidhiano hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya mifuko ya sembe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya makabidhiano hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya ndoo za mafuta ya kula, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya makabidhiano hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, moja ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, Elias Tarimo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto), akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, wakati wa makabidhiano hayo. Katikati ni Naibu Meya wa Ilala, jijini Dar es Salaam, Kheri Kessy.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto), akiwaeleza jambo viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa makabidhiano hayo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Saidi Sadiki, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na kulia ni Naibu Meya wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Songoro Mnyonge.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati), akiwatembeza wageni hao kwenye moja ya kijiji kilichoathirika kwa mafuriko hayo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki.
Daraja la Dumila, lililoathiriwa na mafuriko linavyoonekana baada ya kufanyiwa ukarabati kwa ajili ya kupitisha magari yaendayo Dodoma na Dar es Salaam.
Ukarabati ukiendelea kwenye daraja hilo kwa ajili ya kuliimarisha.
Sehemu ya mto, unaopita kwenye daraja hilo, ukiwa umetanuka kutokana na mafuriko yaliyolikumba eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (wa pili kulia), akiwatembeza wageni wake hao, kwenye daraja hilo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (wa pili kulia), akiwaeleza jambo wageni hao, wakati alipokuwa akiwatembeza kwenye daraja hilo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki.
Hili ni moja ya eneo la Kijiji cha Magore, lililoathirika na mafuriko hayo, wilayani Kilosa hivi karibuni.
Hili ni eneo la Shule ya Msingi, Magore, lililoathirika na mafuriko hayo, wilayani Kilosa hivi karibuni.
Hiki ni Kijiji cha Magore kilichoathirika na mafuriko hayo, wilayani Kilosa.
Wananchi walioathirika kwa mafuriko wa Kijiji cha Magore wakigawana chakula kwenye kambi yao kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na wananchi walioathirika kwa mafuriko wa Kijiji cha Magore, wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, ilipofika mkoani humo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika hao, mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akizungumza na wananchi walioathirika kwa mafuriko wa Kijiji cha Magore, wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, ilipofika mkoani humo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa waathirika hao, mwishoni mwa wiki.
Wananchi wa Kijiji cha Magore, walioathirika kwa mafuriko, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati kamati hiyo, ilipowatembelea na kuongea nao kwenye kambi yao, baada ya kukabidhi misaada mbalimbali.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akizungumza  na Wananchi wa Kijiji cha Magore, walioathirika kwa mafuriko, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, akizungumza katika ziara hiyo, kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Gharib Said Mohammed akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Magore, walioathirika kwa mafuriko, wilayani Kilosa, wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipowatembelea kwenye kambi yao, baada ya kukabidhi misaada yao kwa Mkuu wa Mko, Joel Bendera kwa ajili ya waathirika hao.
Wananchi wa Kijiji cha Magore, walioathirika kwa mafuriko, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati kamati hiyo, ilipowatembelea na kuongea nao kwenye kambi yao, baada ya kukabidhi misaada mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Uslama ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa waathirika hao, kijijini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, akipeana mikono na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo, baada ya kuahidi kutoa mifuko ya Cement 1000 na pia kutoa sh. milioni mbili, fedha taslim kwa watu waliofariki katika mafuriko hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, fedha hizo kwa ajili ya familia za watu waliopoteza maisha kwenye mafuriko hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, naye akizikabidhi fedha hizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo kwa ajili ya kuzifikisha kwa familia za watu waliopoteza maisha kwenye mafuriko hayo.

No comments:

Post a Comment