Wednesday, August 15, 2012

Clinton aipongeza Uganda kwa juhudi za kulinda amani

Hillary Clinton katika ziara yake ya Afrika Hillary Clinton katika ziara yake ya Afrika
Wiki iliyopita, Uganda ilitangaza kwamba itatuma helikopta za kivita nchini Somalia kukiimarisha kikosi cha wanajeshi 17,000 cha Umoja wa Afrika kilichoko nchini humo kupambana na waasi wa Al-Shabaab wenye mafungamano na Al-Qaeda.

Akiwa ziarani nchini Uganda juma lililopita sehemu ya ziara yake ya siku 11 barani Afrika, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton, aliipongeza nchi hiyo kwa mchango wake katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Umoja wa Afrika kushambulia Kismayu
Mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika Mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika
Mbali na Uganda nchi nyengine zinazoshiriki katika kikosi hicho ni Burundi, huku Kenya na Djibuti zikisemekana pia kujiunga.
 Kenya iliingia vitani dhidi ya waasi wa Al-Shabaab ndani ya Somalia mwaka jana baada ya mashambulizi kadhaa ya kiagaidi nchini Kenya ambapo inaaminiwa yalifanywa na waasi hao.
Kikosi cha Umoja wa Afrika kinapanga masahambulizi makubwa katika mji wa kusini wa Kismayu, ambao ni ngome kuu ya Al-Shabaab, kabla ya Agosti 20.
 tarehe hiyo ndipo muda wa serikali ya sasa ya mpito utakapomalizika rasmi. Tayari bunge limepitisha katiba mpya ya muda na hatua hiyo itafuatwa na uchaguzi wa rais pamoja na kuundwa serikali mpya, itakayochukua nafasi ya utawala utakaoamalizika muda wake.

No comments:

Post a Comment