Mabaki ya helikopta mbili za kijeshi za Uganda yamepatikana
katika msitu wa Mlima Kenya. Helikopta hizo zilianguka katika eneo hilo
zilipokuwa njiani kuelekea Somalia.\
"Helikopta zimepatikana lakini zimeungua kabisa," alieleza afisa mmoja
wa jeshi la Kenya. "Hatufahamu hatma ya waliokuwa kwenye helikopta
hizo." Msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri, amethibitihsa
kupatikana kwa mabaki ya helikopta hizo. Juhudi za uokozi bado
zinaendelea. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote juu ya watu kumi
waliosemekana kuwa ndani ya helikopta hizo za kijeshi.
Helikopta nyingine ya jeshi la Uganda, ilianguka Jumapili katika misitu
ya Mlima Kenya lakini wanajeshi saba wa Uganda waliokuwa ndani ya
helikopta hiyo waliweza kuokolewa. Helikopta zote tatu ni za aina ya
Mi-24 na zimetengenezwa Urusi. Zilikuwa zikielekea Somalia kuungana na
majeshi ya Umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la
al-Shabaab. Helikopta nyingine ambayo ni aina ya Mi-17 ilianza safari
Jumapili kuelekea Somalia na kutua salama mjini Garissa, Kenya, ambapo
iliongeza mafuta kabla ya kuendelea na safari.
Mabaki ya Helikopta mbili za Uganda ambazo ziliripotiwa kutoweka siku ya Jumapili zimepatikana mashambani nchini kenya.
No comments:
Post a Comment