Walinzi wa warrior security wakiwa katika mistari wakisikiliza semina /maelekezo mafupi kuhusu uaminifu kazini
field office Paul Mambi kushoto na field office Emmanuel Maganga wakimsikiliza kwa makini Glen Corey.
buti hii imenivutia na kuamua kusimama kupiga picha hakika inapenda sana |
Meneja masoko wa ndani kampuni ya ulinzi ya WARRIOR security yenye makao makuu yake migombani street mikocheni plot no 167 MR GLEN COREY leo mapema asubuhi amewaasa na kuwakumbusha walinzi wa kampuni hiyo kwa kuwa waaminifu /waadilifu kazini ili kulinda heshima yao kwa kutunza mali ya mteja na pia kutunza heshima ya kampuni.
akiongea na walinzi hao katika makao makuu ya warrior security jijini Dar kwa upande wa Tanzania Bwana Glen corey aliweza kuongea na askari hao vizuri juu ya kuwa na uaminifu kwa mali ya wateja na jamii nzima ili kuinua kampuni ambayo kwa sasa inakuwa kwa kasi ikiwa na zaidi ya mikoa kama ARUSHA,TANGA ,MANYARA,DAR ES SALAAM ,KILIMANJARO NA MOROGORO pia katika nchi kama SOUTHERN SUDAN,GOMA HUKO CONGO huku wakisimamia mradi wa kusindikiza magari makubwa ya mizigo kutoka itokayo Zambia kuanzia TUNDUMA hadi Bandari ya SALAMA.
Glen corey aliweza pia kuelezea kuhusu huduma ya NHIF kuwa ni mpango mzuri ambao utawapa wafanyakazi wa Warrior nafasi ya kupata matibabu katika hospitali za serikali na kuwaambia kuwa wasiwe na wasi wsi kwani wako bega kwa bega kuona wanapata mshahara mzuri na wanaishi maisha mazuri.
aidha walinzi hao nao walipata fursa ya kuongea ambapo moja kwa maojawalitoa kilio chao kwa nauli kupanda na kuomba nao waongezewe mishara ili kujikim na maisha na mwisho kabisa walitoa waito kwa jamii kupenda kushirikiana na makampuni ya Ulinzi kama Warrior security pamoja na Jeshi la polisi ili kuzuia na kutokomeza wizi, uharibifu pamoja upotevu wa mali miongoni mwa jamii.
No comments:
Post a Comment