Monday, January 21, 2013

MULIKA HAKI ZA WATOTO


Hiini kampeni  ya kutetea haki za watoto  

Kutokana na kukuthiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto duniani mimi Gasper Sambweti  kama  kijana baba wa familia ya watoto wawili ninaopenda watoto ,nimelazimika kuanzisha kampeni ya MULIKA HAKI ZA WATOTO. Nawashurukuru  wote waliokubali  kuniunga mkono katika kampeni hii
Lengo kuu la kampeni  hii ni kutoa  taarifa kuhusiana na vitendo dhidi ya ukatili kwa watoto  mfano kunyimwa kwenda shule ili aolewe,kupigwa hadi kusababishiwa majereha au vilema,kufukuzwa majumbani,kuuwawa kwa kunyongwa,kutupwa majalalani na chooni,kuchomwa moto na mama/baba wa kambo  ,kunyima haki za msingi kama chakula ,matibabu,malazi ,elimu  na haki za msingi.

Kampeni hii itawahusu watu wote  kuaanzia   vijana  ambao ndio kundi husika zaidi kwani vijana ndio waliotoka katika kundi la utoto na kuwa vijana,pia vijana ndio kundi linaloelekea katika kundi la baba na mama hivyo kama vijana watakuwa katika mstari wa mbele kutafuta haki za watoto basi ni rahisi sana kwa haki hizo kupatikana

Kampeni hii itakuwa na matawi Tanzania nzima ili kuhakikisha haki hizo zinapatikana pia kampeni hii itawahusiha makundi ya wanaharakati pamoja na mashirika yote yanayopambana ili kuhakikisha haki za watoto  zinapatikana.

Wewe ukiwa kama mpenda haki  pia napenda kukuita mwanaharakati naomba tuungane pamoja katika kufichua maovu na ukatili dhidi ya watoto
Kumbuka kama hakuna watoto basi hakuna vijana ,saidia haki za watoto  kujenga nchi yenye viongozi na watu bora.

Kama umevutiwa na waraka huu tadhali ungana nasi katika harakati hizi kwa pamoja tunaweza ,

Unangoja nini muda ni huu jiunge nasi kutokomeza uovu dhidi ya watoto

Kwa habari zaidi fuatilia kundi la facebook;MULIKA HAKI ZA WATOTO
Na ujiunge pale

Pia habari zote za watoto zitakuwa zikichapishwa kwenye blog yetu ya habari na burudani( G SAMBWETI-sambweti.blogspot.com)na kwa baadae tutapata vipindi mbali mbali kuhusiana na haki za watoto katika radio na television  kwa kupitia wahandishi na vijana wote watakao jitolea kupambana na ha haki za binadamu .

Mwisho kabisa tunakaribisha mashirika na watu binafsi watakao vutiwa na harakati hizi kuungana nasi kwa namna yoyote  ile ili kufanikisha kampeni hii na kuhakikisha jamii inafaidika na hili
MAWASILIANO 0 755 656 445/0717 830 580
hapo chini ni wimbo wa kuhasisha utunzaji wa watoto

No comments:

Post a Comment