Rais
wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim (wa pili) na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakitoka
katika eneo la kupumnzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere. Waziri Mpango amemuaga Rais huyo baada ya kuwepo nchini kwa
takribani siku tatu. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt.
Jim Yong Kim (wa pili kushoto) baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi
hapa nchini, ambapo alishiriki uwekaji wa jiwe la Msingi katika ujenzi
wa barabara za juu eneo la Ubungo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (aliyevaa tai) akiwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa kumuaga Rais wa
Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim aliyekuwepo nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiondoka katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kumuaga Rais wa Benki
ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, muda mfupi kabla ndege iliyombeba Rais huyo
kuondoka.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto)
na Afisa mwingine wa Serikali wakishuhudia wakati Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bi. Bella Bird wakibadilishana mawazo baada ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuondoka nchini.
Dar es Salaam, Machi 21, 2017
RAIS
wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, ameondoka nchini baada ya ziara ya
kikazi ya siku tatu na kuagwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es Salaam.
Katika ziara yake ya Siku tatu Dkt.
Jim Yong Kim, pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli, alishiriki
tukio la uzinduzi wa ujenzi wa barabara
ya juu (Ubungo Interchange) katika makutano ya barabara Ubungo
itakayogharimu Sh.188.7 Bilioni kati ya hizo Benki ya Dunia itatoa
Sh186.8 kwa ajili ya ujenzi na usanifu na Sh1.9 Bilioni zitatolewa na
Serikali kwa ajili ya kulipa fidia.
Aidha
umma umeshuhudia utiwaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo itakayo fadhiliwa na Benki ya Dunia hapa nchini,
yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.74.
Miradi hiyo ni ile ya Uboreshaji
Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya
nne ya mradi wa mabasi yaendayo haraka-DART, Mradi wa kusambaza maji
safi, mazingira na ukusanyaji wa maji taka, na mradi wa uendelezaji wa
miji ya Arusha, Dodoma, Tanga, Kigoma, Mwanza, Mbeya, na Mtwara.
Pia
katika ziara hiyo, Dkt. Kim alipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi
Zanaki iliyopo Manispaa ya Ilala, ambayo ni moja ya Shule
zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
No comments:
Post a Comment