Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na wananchi wa eneo la Mpigi darajani (hawapo pichani) na kusisitiza katazo la kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) alipotembelea Mamlaka ya Usafi na
Mazingira Chalinze kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika mto Wami.
Na
Lulu Mussa, Bagamoyo
- Pwani
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameagiza kusitishwa
mara moja kwa shughuli zote za kibinadamu kando kando ya Vyanzo vya maji.
Rai hii imetolewa leo na
Waziri Makamba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika
Mkoa wa Pwani eneo la Mto Mpiji ambao umeathirika kutokana na Uchimbaji wa
mchanga na mmomonyoko wa ardhi unaohatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Waziri Makamba amemuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu kuwaondoa watu wote
waliojenga pembezoni mwa Mto Mpiji na kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ndani
ya siku 30.
" Mkurugenzi hakikisheni kuwa wakazi hao waliovamia eneo la
mto huu na kujenga makazi yao ya kudumu wanaondolewa mara moja"
Alisisitiza Waziri Makamba.
Katika hatua nyingine
Waziri Makamba ametembelea Mto Wami na kusikitishwa na uharibifu mkubwa wa
mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo,
ufugaji na uchimbaji haramu wa madini, upasuaji mbao na uchomaji mkaa
unaopelekea mmomonyoko wa udongo na mchafuko/tope jingi na kusababisha kupungua
kwa uzalishaji wa maji.
Katika kukabiliana na
changamoto zilizoainishwa Waziri Makamba amesema Ofisi yake itaanda kikao kazi
kitakachojumuisha wadau wote muhimu ili kunusuru Mto Wami haraka iwezekanavyo.
"Serikali haiwezi kuwekaza fedha nyingi kwenye mradi mkubwa kama huu na
kuona uharibifu ukiendelea na kuharibu miundombinu, hali hii haikubaliki na
nitachukua hatua za haraka.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) yuko katika ziara ya kikazi katika
mikoa Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida kujionea hali ya
mazingira na changamoto za hifadhi katika mikoa husika.
No comments:
Post a Comment