Thursday, April 27, 2017

NAFASI ZA KUVOLUNTEER KWA MARIPOTA WANAOPENDA KUFANYA KAZI NA TAASISI YA KIDINI YA SALVATION MEDIA

Taasisi ya kidini ya kanisa la Yerusalem mpya inayomiliki redio  inayotambulika kama salvation radio tz  chini ya salvation media ltd

inatangaza nafasi kwa waandishi wa habari mikoani wenye  moyo na mzigo wa kumtumikia Mungu kwa njia ya habari.

uongozi wa salvation media unatangaza nafasi za uwakilishi (repota )kwa mikoa yote Tanzania  katika kuripoti matukio mbali mbali ya habari  kwa kuvolunteer

faida za kuvolunteer ni kuongeza wigo wako wa habari,na baadae tunaweza kukuajiri  kama utafikia viwango na kutimiza masharti ya taasisi

kuomba nafasi ya kuvolunteer :
@BARUA YA KUOMBA
@CV
@VIVULI VYA VYETI VYAKO
@DEMO

Tuma kwa  meneja salvation media ltd,
 salvation radio tz  P.O.BOX 408 ARUSHA
email:salvationradiotz@gmail.com

mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/5/2017


SALVATION RADIO TZ

NI redio ya kidini iliyoanzishwa tarehe 01/5/2016 inasikika dunia nzima kwa njia ya internet  inavipindi mbali mbali  na inarusha matangazo yake kutoka jijini Arusha Tanzania

salvation radio tz ni redio ya kanisa  tarehe 01/05/2017 itatimiza mwaka mmoja tangu  kuanzishwa na  sababu hiyo ndio sababu kuu ya kutangaza nafasi hizi ili kutoa fursa kwa wale wenye nia ya kumtumikia Mungu

uongozi wa salvation media  unakaribisha sana maombi yenu kwa nafasi iliyotangaza  vigezo na mashrti vitazingatiwa katika  kupokea volunteer hao.

imetolewa na

meneja wa redio salvation .

27/4/2017

UNAWEZA KUSILIZA SALVATION RADIO POPOTE KWA KUBONYEZA HAPA salvationradiotz.listen2myshow.com 

au unaweza kupakua app ya streema radio kisha search salvation radio tz play na usikilize kokote ulipo duniani

No comments:

Post a Comment