Tuesday, April 11, 2017

SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI


Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango huo .

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akipokea vitanda hivyo kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy , kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi.

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy , kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi.wakikagua vitanda hivyo mara baada ya makabidhiano.






Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitanda vya hospitali nchi nzima uliofanyika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma leo katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi 
 
 
……………………………………………………………………..
Serikali ya awamu ya tano nchini imezindua rasmi usambazaji wa vifaa vya hospitali kwa halmashauri zote nchini katika kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za afya nchini kwa kuhakikisha wananchoi wanapata huduma kwa kiwango stahiki 

Akizindua usambazaji huo leo wilayani hapa,Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi iliyotoa kwa wananchi ambapo serikali inawekeza katika afya ya wananchi hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda 

Akizungumza kwenye hadhara ya wanachi wa Wilaya ya Kongwa,Waziri Ummy alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17. 

“Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya,hivyo wanaomba wananchi kuhakikisha mnafika kwnye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata matibabu sahihi” 

Aidha, Waziri Ummy alisema kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya Umma ,Wizara yake kwa bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga kiasi cha shilingi biliuoni 4 za kuwezesha kununua pamoja na kusambaza vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini
Alivitaja vifaa vilivyonunuliwa na kuvikabidhi kwa Mhe. Job Ndungai (Mb), Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania Mhe. John Ndugai ni pamoja na vitanda vya hospitali (20),vitanda vya kujifungulia wajawazito (5), magodoro (25) na mashuka (50). 

Vifaa vya Hospitali vitakavyopasambazwa kwenye Halimashauri zote 184 nchini ni pamoja na vitanda vya hHospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia akinamama wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200. Thamani ya vifaa hivi ni shilingi bilioni 2,933, 125,600. Zoezi la kugawa vifaa hivi linatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30, 2107. 


Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Ndugai ameishukuru Serikali kwa msaada wa vifaa vilivyotolewa kwa Hospitali na vituo vya Afya katika mkoa wa Dodoma ikiwemo Halmashauri Kongwa. Vifaa hivyo vitaboresha afya ya wananchi wa jimbo la Kongwa na maeneo mengine nchini na hivyo kusaidia kuwawezesha wananchi kukutumia mudao wao mwingi katika shughuli za kiuchumi.

No comments:

Post a Comment