Wednesday, May 17, 2017

Mchanganuo wa rambirambi za wanafunzi Lucky Vicent watolewa!



Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema anasikitishwa na baadhi ya  viongozi wa kisiasa ambao wamelichukulia suala la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kisiasa.

 Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Gambo amesema  uongozi wa mkoa wa Arusha umeamua kutoa taarifa ya wazi kwa yumma kuhusu michango iliyotolewa na matumizi yake.

“Hili si tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamotyo kubwa uliozikumba familia za wananchi wetu. Wakati serikali inahangaika na shida za watu tunasikitika kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa wanahangika na mitandao ya kijamii,”imesema taarifa hiyo

 Taarifa hiyo iliyoambatana na jedwali lenye mchanganuo wa rambi rambi hizo inaonyesha kuwa jumla ya michango ya serikali na ya wadau ni Sh 261.3 milioni.

Michango ya  Serikali ni Sh 102.7milioni na ya wadau ni Sh 158.5milioni.

 Katika mchanganuo wa taarifa hiyo, Gambo amesema familia za  wafiwa hao zitapewa Sh 3,857,143 kwa kila familia. Kila familia ilipewa Sh1milioni siku ya kuaga miili uwanja wa Sheikh Amri  Abeid.

No comments:

Post a Comment