Monday, June 19, 2017

Aliyemuua waziri Somalia ahukumiwa kifo

Abas Abdullahi Sheikh
Image captionAbas Abdullahi Siraji alikuwa waziri wa umri mdogo zaidi Somalia
Mwanajeshi wa Somalia aliyempiga risasi na kumuua waziri wa umri mdogo zaidi aliyewahi kuteuliwa nchini Somalia amekuhukiwa kuuawa kwa kupigwa risasi.
Abas Abdullahi Siraji aliuawa mwezi uliopita akiwa ndani ya gari lake karibu na ikulu ya rais mjini Mogadishu.
Anadaiwa kuuawa na Ahmed Abdullahi Abdi, aliyemdhania kuwa mwanamgambo wa Kiislamu kimakosa.
Wengi walighadhabishwa na kuuawa kwa waziri huo.
Mahakama ya kijeshi imemhukumu kifo mwanajeshi huyo, lakini anaweza akakata rufaa.
Mawakili wa mwanajeshi huyo wanasema mauaji hayo yalikuwa ajali, shirika la habari la AFP limeripoti.
Wanasema gari la waziri huyo liliwafanya walishuku kutokana na hali kwamba lilikuwa linalifuata gari la mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, ambaye mwanajeshi huyo alikuwa anamlinda.
Gari likiwa na risasiHaki miliki ya pichaAFP
Siraji, 31, aliibuka kuwa mbunge wa umri mdogo zaidi katika bunge la Somalia Novemba mwaka jana kabla ya kuchaguliwa kuwa waziri wa ujenzi mapema mwaka huu.
Aliishi kama mkimbizi nchini Kenya na alikuwa mfano wa kuigwa na alienziwa na wengi kutokana na bidii yake na kujitolea kufanikiwa.
Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alimteua kuwa waziri.
Baada ya kuuawa kwake, rais alikatiza ziara yake Ethiopia na kurejea nyumbani kuhudhuria mazishi yake.
Burial of Abas Abdullahi Sheikh
Image captionRais Farmajo alihudhuria mazishi ya Siraji

No comments:

Post a Comment