Monday, June 19, 2017

Champs Elysees: Gari la polisi lagongwa Paris

Paris, France, 19 Juni 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAfisa wa polisi akikimbia kuelekea kwenye gari hilo barabara ya Champs Élysées
Gari moja limeendeshwa makusudi na kugonga gari la polisi katika eneo la kifahari la Champs Élysées, katikati mwa Paris, maafisa wa polisi wamesema.
Gari hilo lilishika moto muda mfupi baadaye.
Dereva wa gari hilo amefariki.
Polisi wamepata bunduki aina ya Kalashnikov ndani ya gari hilo, bunduki nyingine kadha za kawaida na chupa zenye gesi.
"Maafisa wa usalama wamelengwa tena kwenye shambulio Ufaransa," waziri wa mambo ya ndani Gerard Collomb amesema, na kulitaja kuwa "jaribio la shambulizi".
Hakuna raia au maafisa wa usalama waliojeruhiwa.
Ufaransa kwa sasa imo katika hali ya hatari baada ya kutokea kwa msururu wa mashambulio miaka ya akribuni.
Polisi aliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili wakajeruhiwa katika shambulio Champs Élysées Aprili, siku chache kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.
Kisa cha sasa kimetokea siku moja baada ya uchaguzi wa ubunge nchini Ufaransa, ambapo chama cha Rais Emmanuel Macron kilipata ushindi mkubwa.
Paris, Ufaransa, 19 Juni 2017.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wa kutegua mabomu wakikagua gari lililogongeshwa kwenye gari la polisi
Champs-Elysees 19 Juni 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionFoleni ya magari iliyosababishwa na operesheni ya kiusalama eneo hilo
Champs-Elysees avenue in ParisHaki miliki ya pichaAFP

No comments:

Post a Comment