Wednesday, June 7, 2017

MBUNGE COSATO CHUMI ATOA MSAADA WA AMBULANCE NYINGINE JIMBONI KWAKE

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi
 akizungumza na wananchi wa Igohole wakati kukadhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amepewa na wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole
 hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi kwa kushirikiana na wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Na Fredy Mgunda,Mafinga


MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi kwa kushirikiana na wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la
kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole
ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.
 
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa
uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho
katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.
 
Akikabidhi msaada huo Chumi alisema;
“napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika
mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”
 
Alisema gari hilo la wagonjwa
ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza
kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.
 
Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi
ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha
vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha jimbo la mafinga
mjini linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.
 
Akishukuru kwa msaada huo, Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya
msaada huo, kituo hicho cha afya kilikuwa hakina gari hata moja la kubeba
wagonjwa.
 
“Pamoja na kuhudumia hospitali hiyo
ya wilaya, kurikuwa na magari mawaili tu ambayo yalikuwakihudumia vituo vingine
18 vya kutolea huduma katika wilaya hiyo hivyo,” alisema Mhagama.
 
Alisema kupatikana kwa gari hilo
jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo  kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na
maisha ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.
 
Akizungumzia huduma ya mama na mtoto
katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama alisema kwa wastani wajawazito 500
wanajifunga kila mwezi hospitalini hapo.
 
“Kati yao wajawazito zaidi ya 100
huwa wanapata huduma za dharula huku wastani wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma
za rufaa,” alisema dr Mhagama.
 
Naye
mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema halmashauri
yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali
zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na
madiwani ili kuboresha huduma kwa watu wake.

No comments:

Post a Comment