Thursday, June 1, 2017

Rais wa Afghanistan alaani shambulizi lililouwa watu 90

Shambulizi hili linatajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo
Image captionShambulizi hili linatajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameelezea shambulizi la bomu katika mji mkuu Kabul kama uhalifu dhidi ya ubinaadam.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres pia amelaani shambulizi hilo lililouwa watu 90.
Zaidi ya watu 400 walijeruhiwa.
Dereva wa BBC Mohammed Nazir, ni miongoni mwa waliouawa.
António Guterres pia amelaani kitendo hicho
Image captionAntónio Guterres pia amelaani kitendo hicho
Polisi nchini humo wanasema kuwa kundi la mtandao wa Haqqani ambalo lina uhusiano na Taliban linahusika katika tukio hilo likishrikiana na Pakistan.
Taliban na Pakistan kwa pamoja wamekanusha kuhusika.

No comments:

Post a Comment