Mamilioni ya watu leo watapiga kura kwenye uchaguzi mkuunchini Uingereza.
Shughuli ya upiganji kura itaaza mwendo wa saa moja asubuhii saa za Uingereza wakati zaidi ya vituo 40,000 vitafunguliwa kote nchini.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.
Ni ongezekao kutoka uchaguzi wa mwaka 2015 wakati wapiga kura milioni 46.4 walikuwa wamejiandikisha.
- Bunge Uingereza launga mkono uchaguzi wa mapema
- Uingereza yaanza rasmi kujiondoa EU
- Shirika la ujasusi Uingereza lakana kumdukua Trump
- Bi.May ataka utulivu wa kisiasa Uingereza
Kura zingine tayari zimepigwa kupitia kwa posta ambayo ilichukua asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.
Vituo vingi vya kupigia kura viko shuelni na katika vituo vya kijamii.
Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa mchana.
No comments:
Post a Comment