Thursday, June 1, 2017

Urusi yawafukuza wanadiplomasia wa Moldova

Waziri mkuu wa Moldova Pavel Filip amesema kulikua na sababu maalum za kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi
Image captionWaziri mkuu wa Moldova Pavel Filip amesema kulikua na sababu maalum za kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi
Urusi wamewafukuza wanadiplomasia watano wa Moldova, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa Moldova kufukuza idadi sawa ya wafanyakazi wake wa kidiplomasia siku ya Jumatatu.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema ina matumaini Moldova alijua faida kubwa ya matendo yake.
Moldova haikutoa sababu za kufukuzwa kwa wanadiplomasia hao licha ya kwamba hakukua na mvutano wowote baina ya pande hizo mbili.
Urusi inasema iwapo Moldova itatoa sababu inayoeleweka basi kuna uwezekano wa kusawazisha mambo.

No comments:

Post a Comment