Polisi nchini Kenya wanachunguza ghasia katika shule ya upili ya umma ambapo wanafunzi kadhaa walidungwa visu kutokana na madai ya ubaguzi wa kidini .
Ghasia za wanafunzi sio jambo geni lakini kile ambacho kimewawacha wengi mdomo wazi ni vile wanafunzi hao walivyofanikiwa kuingia katika shule hiyo wakiwa na visu na mapanga.
Kulingana na mwandishi wa BBC Mercy Juma shule ya upili ya Jamhuri iliopo katika mtaa wa jiji la Nairobi imefungwa mara moja na wanafunzi walio zaidi ya 1,500 kurudishwa nyumbani.
Haijulikani ni nini hasa kilichosababisha ghasia hizo za Jumanne usiku ambazo ziliwawacha wanafunzi saba na majareha katika vita vilivyohusisha visu na mapanga.
- Rais Zuma amfuta kazi waziri wa elimu ya juu
- Rais wa Hungary apitisha sheria tata ya elimu
- Mfalme wa Zulu aunga mkono adhabu ya kiboko shuleni
Afisa mkuu wa jiji la Nairobi Japeth Koome anasema kuwa wameanzisha uchunguzi dhidi ya madai ya utaratibu wa kidini katika shule hiyo.
Vyombo vya habari nchini humo vina habari kwamba vita hivyo vilizuka baada ya baadhi ya wanafunzi kupinga kuhusu upendeleo wa kidini unaodaiwa kutekelezwa na wakuu wa shule hiyo.
Wakenya katika mitandao ya kijamii wameshangazwa na vile silaha kama vile visu na mapanga zilivyoingia katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment