Wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Syria wanasema kwa siku kumi mfululizo,vikosi vya serikali ya Syria vimekuwa vikishambulia hospitali katika maeneo yanayokaliwa na waasi nchini humo.
Mshauri wa masuala ya afya wa umoja wa mataifa aliyepo nchini humo Hamish de Bretton-Gordon mashambulizi hayo yanarudisha nyuma juhudi zao za kuwapatia watu huduma za afya.
Anasema hospital zimeharibiwa vibaya Mashariki mwa mji wa Ghouta na Damascus,na jimbo la Kaskazini la Idlib.
Bretton-Gordon amesema zaidi ya watoto 150 wanahitaji kuondolewa katika maeneo hayo ili kupata huduma kamili za afya.
Hali ya usalama nchini Syria imekua ya kuzorota kila kukicha kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali na washirika wake dhidi ya waasi wanaopinga serikali ya Rais Bashar al-Assad.
No comments:
Post a Comment